Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017
amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Balozi mmoja.
Wabunge
walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan
Mwaluko Kabudi.
Wabunge wateule
hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.
Kituo cha kazi na
tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa
baadaye.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni