JESHI la Polisi Mkoani Geita limesema linamshikilia Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Edward Lowassa kwa mahojiano.
Akizungumza na Daily News/Habarileo Online, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alikiri kumshikilia kiongozi huyo aliyepata kuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema aliyeungwa mkono na UKAWA, na kusema kuwa atatoa taarifa kamili baada ya kumaliza mahojiano nae.
Taarifa za awali kutoka Geita zinasema kuwa Lowassa alikamatwa mkoani Geita alipokuwa akisalimia wananchi wakati akitokea Mkoani Kagera katika ziara na alikuwa njiani kwenda katika Kampeni Kata ya Nkome Geita Vijijini.
Mbali na Lowassa pia Polisi inamshikilia Mbunge wa Viti Maalum Geita, Upendo Peneza na watu wengine kadhaa ambao walikuwa msafara mmoja na Kiongozi huyo wa Chadema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni