Jumapili, 22 Januari 2017

NAMAINGO YAZINDUA MRADI MKUBWA WA KUKU WA KIENYEJI LINDI

 Wakiwa na furaha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Namaingo Business Agency Limited, Ubwa Ibrahim baada ya kuzindua Mradi wa Ufugaji  Kuku kwa wanachama 3000 wa kampuni hiyo kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Miteja, wilayani humo juzi O.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Abuu Mjaka akifungua mlango katika banda la vifaranga vya mbegu vya mradi huo
 Vifaranga vya mbegu ya kuku wa kienyeji vinavyofugwa kisasa
 Mpiga Picha wa Gazeti la Tanzania Daima,  Said Powa ambaye aliliwakilisha kundi la Wananchama Wanahabari la Kwanza One akipokea cheti cha usajili kutoka kwa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Mjaka wakati wa hafla hiyo
 Kundi la Wanahabari la Kwanza One likishangilia kwa furaha baada ya kukabidhiwa cheti cha kuwa miongoni mwa wanachama watakaoshiriki kwenye mradi huo
 Mbegu za mazao zilizooteshwa kwa ajili ya kulisha kuku

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Ufugaji Kuu ya Shitindi Poutry Farm, Shitindi (katikati) akizungumza wakati wa uzinduzi, ambapo aliahidi kununua mayai ya wanachama wa ufugaji wa kuku wa Namaingo.


 Ni burudani kwa kwenda mbele
 Mtalaamu wa ufugaji kuku wa kienyeji akielezea jinsi mfugaji anavyoweza kuzalisha majani ya malisho kwa kutumia mazao mblimbali

 Mkurugenzi Mtendaji wa Namaingo, Ubwa Ibrahim akizungumza wakati wa hafla hiyo
 Sehemu ya umati uliohudhuria hafla hiyo
 Mjaka akihutubia wakati wa hafla hiyo
 Baadhi ya Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba
 Moja ya mabanda ya kuku yaliyoandaliwa kwa ajili ya
Wanachama wakifurahia baada ya kukabidhiwa cheti cha usajiri wa Biashara cha Brela


Mwenyekiti wa Namaingo Mkoa wa Ruvuma akipokea cheti cha Brela
Dk. Hassan Kijaki Mtaalalamu wa Mifugo wa Mkoa wa Lindi akielezea kufurahishwa na kitendo cha Namaingo kuwekeza mradi wa kuku mkoani humo.
Mchumi wa Mkoa wa John Mwalongo akihutubia wakati wa hafla hiyo
Bi Ubwa na Mjaka wakikagua bidhaa mbalimbali za wAJASIRIAMALI ZILIZOFUNGWA KWA NJIA YA KISASA


Jumatatu, 16 Januari 2017

MBIO ZA KILIMANJARO MARATHON 2017 ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KILIMANJARO.

Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 zimezinduliwa leo Mjini Moshi katika mkutano na wanahabari ulioandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na wadhamini wengine.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli, Aliyewakilishwa na Meneja Mauzo wa TBL Kaskazini, Richard Temba,  alisema mbio hizo zitafanyika Februari 26, 2017 wilayani Moshi na zitahusisha wanariadha wa ndani na nje ya nchi kutoka pande mbalimbali za dunia.


“Kilimanjaro Premium Lager imeingia mwaka wake wa 15 kama mdhamini mkuu wa mbio hizi, kwa mafanikio makubwa na kuzifanya kuwa moja ya mbio kubwa zaidi za marathon barani Afrika, kwani kwa sasa hujumuisha zaidi ya wanariadha 8,000 kutoka nchi zaidi ya 45 kote duniani,” alisema Kikuli.

Kwa mujibu wa Meneja huyo wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Tigo kwa 21km, Gapco kwa 10 km-viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt-5km. Wadhamini wengine ni pamoja na KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Keys Hotel na pia wadhamini wapya Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Alisema Kilimanjaro Premium Lager imewekeza zaidi ya Tsh milioni 500 katika mashindano haya na washindi  katika mbio za kilomita 42 watapata milioni 4 kila mmoja upande wa wanaume na wanawake huku jumla ya zawadi ikiwa Milioni 20.


Akizindua mbio hizo Mjini hapa,Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba aliwapongeza Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wengine na waandaaji kwa kazi nzuri kila mwaka, akiongeza kuwa mashindano yametokea kuwa moja ya matukio makubwa zaidi ya kimichezo ndani na nje ya nchi.

“Mashindano haya pia yamekwenda mbali zaidi katika kukuza utalii kwani wanariadha wa kimataifa na wageni wao hufanya utalii baada ya mashindano na hiyo kufaidisha uchumi wa nchi,” alisema huku akisisitiza kuwa mbio hizo zitatoa fursa nyingi sana hasa za kibiashara.

Mkurugenzi  wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata , alisema huu ni mwaka wao wa tatu mfulululizo wa udhamini wa mbio za kilomita 21 na kuwa wamepata mafanikio makubwa kutokana na udhamini huu  kutokana na mashindano haya kukua mwaka hadi mwaka.

Alisema mwaka huu wamejiandaa vizuri na watatumia mbio hizi kuhamasisha uhifadhi wa Mlima Kilimanjaro ili uendelee kuingizia fedha nyingi za kigeni kutokana na utalii huku akiongeza kuwa nia yao pia ni kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuleta mafanikio katika riadha na kuiweka Tanzania katika ramani nzuri ya kimichezo.

Kwa mujibu wa Bw. Lugata, jumla ya zawadi watakaotoa kwa washindi wa mbio hizo ni Tsh milioni 11.

Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania Caroline Kakwezi alisema kwa mara nyingine watatoa usafiri, malazi na chakula kwa washiriki wa mbio za kilometa 10 kutoka Dar es Salaam na usafiri kwa washiriki kutoka Arusha na Moshi.

Kakwezi alisema, “Tanzania Paralympic Committee imeandaa shidano la mchujo ili kuwapata washiriki wa Kilimanjaro Marathon na mchujo huu utafanyika katika Uwanja wa Uhuru Jumamosi Februari 11 kuanzia saa mbili kamili. Tunawaomba washiriki wote wajitokeze ili waweze kupata nasfasi hii,” alisema huku akiwashukuru wateja wa GAPCO kwa kuendelea kuwaunga mkono na kuwawezesha kudhamini Kilimanjaro Marathon kwa miaa sita sasa na kuongeza kwamba jumla ya zawadi watakazotoa kwa washindi ni Tsh milioni 10.4.

Meneja wa Grand Malt, Oscar Shelukindo alisema wanaona fahari kubwa kudhamini mbio za kilometa tano na kuwataka wale wote wanaoona hawataweza kushiriki kwenye mbio ndefu kujitokeza kwenye mbio hizo za umbali wa kilometa tano, akisema zina mvuto wa aina yake.
Alisema Grand Malt imepata mafanikio makubwa kutokana na matukio kama haya kwani ni kinywaji chenye afya cha watu wa rika zote.

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MWANDISHI WA HABARI ZA MICHEZO AMINA ATHUMAN DAR

 Waombolezaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, Amina Athuman  walipokuwa wakioutoa nyumbani kwake Banana, Dar es Salaam leo, kuliingiza kwenye gari tayari kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Lushoto kwa mazishi. 
 Mwili wa aliyekuwa Mwandishi wa Habari za Michezo wa Gazeti la Uhuru, marehemu  Amina Athumani ukiombewa dua nyumbani kwake, Banana, Ukonga.
 Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto (kushoto) akimzungumzia marehemu Amina kuhusu uchapakazi wake enzi za uhai wake
 Baadhi ya waombolezaji wakiwemo wanahabari wakiwa eneo la msiba nyumbani kwa marehemu Amina Athuman, Banana, Ukonga Dar es Salaam
 Mwili ukpelekwa kwenye gari
 Mhariri Msanifu Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, ambaye kabla ya kujiunga na gazeti hilo alikuwa Mhariri Mtendaji wa gazeti la Uhuru,Joseph Kulangwa (kushoto), na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania, Juma Pinto wakiwa na huzuni wakati jeneza lenye mwili wa Amina Athuma likitolewa ndani tayari kusafirishwa kwenda Lushoto. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 

HABARI YA HIVI PUNDE!! LOWASSA ASHIKILIWA NA POLISI MKOANI GEITA KWA MAHOJIANO

JESHI la Polisi Mkoani Geita limesema linamshikilia Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Edward Lowassa kwa mahojiano.

Akizungumza na Daily News/Habarileo Online,  Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo alikiri kumshikilia kiongozi huyo aliyepata kuwa Mgombea wa Urais kwa tiketi ya Chadema aliyeungwa mkono na UKAWA, na kusema kuwa atatoa taarifa kamili baada ya kumaliza mahojiano nae. 

Taarifa za awali kutoka Geita zinasema kuwa Lowassa alikamatwa mkoani Geita alipokuwa akisalimia wananchi wakati akitokea Mkoani Kagera katika ziara na alikuwa njiani kwenda katika Kampeni Kata ya Nkome Geita Vijijini.

Mbali na Lowassa pia Polisi inamshikilia Mbunge wa Viti Maalum Geita, Upendo Peneza na watu wengine kadhaa ambao walikuwa msafara mmoja na Kiongozi huyo wa Chadema.

RAIS MAGUFULI AMTEUA BULEMBO NA KABUDI KUWA WABUNGE

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 16 Januari, 2017 amefanya uteuzi wa Wabunge wawili wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Balozi mmoja.

Wabunge walioteuliwa ni Alhaji Abdallah Majula Bulembo na Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Wabunge wateule hawa wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.


Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba itatangazwa baadaye.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016

DC KAKONKO ALITAKA BARAZA LA MADIWANI KUBUNI VYANZO VIPYA VYA MAPATO AMBAVYO HAVIWAUMIZI WANANCHI

MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagaraakizungumza katika kikao Cha Baraza la Madiwani Wilaya ya Kakonko, mkoani Kigoma.
Baadhi ya Madiwani wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Kakonko.
Na FK Blog Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagara ameliomba baraza  la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko  na Mkurugenzi  kubuni vyanzo ambavyo havita waumiza wananchi katika uchangiaji na kuwashirikisha Wananchi katika Shughuri za maendeleo ilikuhakikisha bajeti iliyo pangwa ya mwaka 2017-2018 inafanikiwa kwa asilimia 88% ya bajeti iliyopangwa kwa ukusanyaji mapato ipasavyo.

Pia aliwaomba Madiwani wa upinzani kuacha tabia ya kupinga rasimu ya pendekezo la bajeti iliyopendekezwa ya mwaka 2017-2018 pasipokuwa na hoja ya msingi ikiwa ni pamoja na kupinga kodi ya majengo ya kila mwananchi kuchangia kiasi cha shilingi 5000 kwa mwaka hali inayopelekea halmashauri hiyo kushindwa kuwa na vyanzo vingi vya mapato.

Rai hiyo aliitoa Jana (Leo) katika kikao cha baraza la  madiwani cha kuipitia na   kupitisha rasimu ya bajeti inayo pendekezwa na balaza hill ambapo Ndagara aliwaomba madiwani kuwashawishi Wananchi kuchangiq shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kuchangia Ujenzi wa  vyumba vya madarasa na kuchangia michango mingine iliyopendekezwa kwenye rasimu ilikufikia lengo la kukusanya mapato kwa asilimia 80%.

Aidha Ndagara aliwaomba madiwani kwa kushirikiana na Mkurugenzi kubuni vyanzo vipya vya mapato ya ndani ilikuepuka viporo vilivyo baki kwa bajeti ya mwaka uliopitq ambapo halmashauri hiyo ilishindwa kufikia lengo na kukusanya mapato kwa asilimia 28% kutokana na kukosekana kwa vyanzo vipya vya mapato katika Wilaya.

"Ushauri wangu katika baraza hili  kwenye hii bajeti mlio ipitisha nilazima kuwa na vipaumbele ilikuepuka hivi vipolo vilivyo baki niungane na Afisa mipango, tuwqshirikishe Wananchi kwa nguvu kubwa na tuache kuitegemea serikali siku zote lazima tukusanye kodi ilikuweza kuipatia halmashauri mapato kuacha kuweka vipingamizi visivyo kuwa na msingi ", alisema Kanali Ndagara.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Lusubiro Mwakabibi aliwaomba madiWani kuikataa bajeti kwa hoja ya msingi, kupinga suala la kila mwananchi kuchangia shilingi 5000 kwa mwaka ni kupinga maendeleo hakuna mwananchi anaeweza kukosa kiasi hicho cha hela kwa mwaka suala la  msingi tuongeze vyanzo vya ukusanyaji wa mapato.

Mwakabibi alisema Madiwani wanatakiwa kuwaelimisha Wananchi juu ya ulipaji modi na kuchangia  mapato ya serikali, halmashauri ya kakonko ni halmashauri ya mwisho katika ukusanyaji wa mapato nchini kutokana na vyanzo vidogo vya ukusanyaji mapato halmashauri baada ya kuliona hill imeandaa vyanzo vipya vya mapato ilikuhakikisha mapato yanaongwezeka.

Nae Mwenyekiti wa halmashauri ya Kakonko Juma Maganga alisema halmashauri imeandaa bajeti ya shilingi bilioni 29.7 iliyopitishwa na madiwani  ya mwaka wa fedha 2017 -2018 itakayo husisha makusanyo ya mapato ya ndani na fedha kutoka Serikali kuu itakayo saidia kukamilisha shuguli za maendeleo ya halmashauri hiyo.